Sunday, September 23, 2018

SIMBA SC YAREKEBISHA MAKOSA..YAICHAPA MWADUI FC 3 - 1

  Malunde       Sunday, September 23, 2018


Na Magdalena Kashindye - Malunde1 blog
Simba SC imeibuka  na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mwadui FC mchezo wa Ligu Kuu uliofanyika leo Jioni Septemba 23,2018 katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga na kuwafanya wachimba madini wa Mwadui kuendelea kuchechemea mkiani.
Mabao pekee ya Simba yamewekwa kimiani na Nahodha John Bocco akiweka kambani mara mbili mnamo dakika ya  41 kwa njia ya penati iliyotaka na kufanyiwa madhambi eneo la hatari kisha kufunga tena dakika ya 45.

Bao la tatu la Simba limefungwa na  Meddie Kagere katika dakika ya 51 ya kipindi cha pili na kumfanya afikishe jumla ya mabao manne msimu huu tangu uanze huku John bocco akifikisha magori 100 kwenye ligi kuu bara.

Bao pekee la Mwadui FC lilipachiwa kiminiani na Charles Ilanfya katika dakika ya 82 kipindi cha pili ikiwa ni mapema baada ya Nahodha wa Simba, John Bocco kupewa kadi nyekundu iliyotokana na kumpiga ngumi mchezaji wa Mwadui FC.

Simba ataanza maandalizi kwa ajili ya mchezo mwingine Septemba 30 dhidi ya Yanga.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post