Monday, September 24, 2018

SAKATA LA AJALI YA MV NYERERE: RAIS MAGUFULI,AVUNJA BODI NYINGINE...AMTUMBUA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI SUMATRA

  Malunde       Monday, September 24, 2018
Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Mhandisi Dkt. John Ndunguru na kuivunja bodi hiyo kuanzia leo Septemba 24, 2018.Rais Magufuli amechukua hatua hiyo kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 na matukio mbalimbali ya ajali za barabarani hapa nchini yanayosababisha vifo, ulemavu na uharibifu wa mali.


Pamoja na hatua hiyo kamati ya uchunguzi ambayo itatangazwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa baadaye leo, itaendelea na uchunguzi wa ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kama ilivyopangwa.


Utenguzi huu wa Rais Dkt. John Magufuli ni wa pili kuufanya tokea ilipotokea ajali ya kivuko cha Mv. Nyerere na kusababisha takribani ya watu 224 kufariki dunia kutokana na ajali hiyo.


Jana Septemba 23, 2018 Rais Magufuli aliivunja Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) iliyokuwa chini ya Brigedia Jenerali Mstaafu, Mabula Mashauri kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post