NAPE NNAUYE APATA AJALI YA GARI

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akilitumia aina ya Land Cruiser VX (nyeupe) lenye namba za usajili T349 DEL, kupata ajali na kupindukua asubuhi ya leo Septemba 24, 2018.

Nape amepata ajali hiyo wakati alipokuwa anaelekea wilayani Liwale kuungana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa Dkt. Bashiru Ally anayezuru wilayani Liwale


Aidha, inadaiwa hakuna madhara makubwa yaliyotokea kwa waliokuwa ndani ya gari ambapo kwa sasa Mbunge Nape amepatiwa usafiri mwingine ili kusudi aweze kuendelea na safari yake ya kuelekea wilayani Liwale.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema wameanza kuchunguza chanzo cha ajali hiyo licha ya kuwa eneo lililotokea ajali hakuna hitilafu ya aina yoyote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527