KABEHO ASISITIZA UFUGAJI WENYE KULETA TIJA KWA WANANCHI WA MONDULI.

Wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Monduli Mh: Idd Hassan kimanta akishuhudia Kiongozi mbio za mwenge wa uhuru Ndg Charles Kabeho akiweka jiwe la msingi Shule ya msingi manyara ranchi katika kata ya esilalei

Na Imma Msumba, Monduli

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ndg: Charles Kabeho alipo zuru shamba la mifugo Manyara ranchi lenye ukubwa wa ekari 45000 lililo anzishwa mnamo mwaka 1959 na muekezaji kutoka ujerumani.

Ambapo shamba hilo lilotolewa na serikali na kumilikishwa kwa wananchi wa vijiji vya Esilalei na Oltukai.

kwa mujibu wa taarifa ya shamba hilo iliwasilishwa na afisa mifugo wa shamba ndg lemay  Kibiriti imebainisha kuwa zaidi ya mifugo 1,273,ng'ombe wakiwa 829 na  kondoo 444.

Kwa upande wa shirika la African Wildlife Foundation (AWF) ambao ndio wahisani wa shamba hilo kwa muda mrefu wameendelea kutoa ushirikiano na wakazi wa vijiji hivyo katik shughuli za kimaendeleo kwa maslahi ya wananchi.

Afisa mifugo huyo wa shamba la mifugo (manyara ranch) amesema kuwa lengo la shamba hilo ni kuboresha mifugo ya asili iliwa sambamba na uhamasishaji wa ufugaji wa kibiashara kwa kutumia mbegu bora za mifugo aina ya Boran na kondoo.

Amesema shamba hilo la mifugo lina kadiriwa kuwa na thamani ya shilingi 501,130,000 ambapi shilingi 397,530,000 ni makadirio ya mifugo, huku kwa upande wa miundombinu ikitajwa kufikia shilingi 103,600,000.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527