MAKONDA : NIMESHTUKA SANA...HAUKUWA MPANGO WA MKOA


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda ameagiza mgambo waliopiga raia katika eneo la Bunju mkoani humo kuchukuliwa hatua kali kwani walichokifanya haukuwa mpango wa mkoa.

Akiongea leo jioni Makonda amekemea vikali kitendo hicho ambacho kimefanyika kwenye ofisi ya mtendaji wa kata ya Bunju ambapo mgambo hao wamepiga raia na kuwajeruhi akiwemo mfanyabiashara, Robson Orotho mkazi wa Bunju kutokana na kushindwa kulipa Sh. 50,000 ya taka. 

''Nimeshtuka sana baada ya kuona video hiyo sio kitendo cha kufanywa na watendaji kwani lengo letu ni kusimamia usafi na si kupiga raia, nalaani kitendo hicho na naagiza hatua kali zichukuliwe dhidi yao'', amesema.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni Jumanne amesema Murilo tayari wanawashikilia mgambo watatu wa manispaa hiyo ambao wamehusika katika tukio hilo na taratibu za kisheria zinaendelea na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Muliro amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Goodluck Festo, Rehema Nyange na Kelvin Edson, ambao wote ni mgambo wa manispaa hiyo huku akibainisha kuwa mfanyabiashara huyo anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala.

Siku za hivi karibuni zimesambaa picha za video katika mitandao ya kijamii zikionyesha mgambo wakitoa kipigo kwa watu na kuzua taharuki, wengi wakiwa ni wafanyabiashara ndogondogo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527