MWILI WA KING MAJUTO KUAGWA LEO KARIMJEE, KUZIKWA KESHO IJUMAA TANGA


Mwili wa Mwigizaji Mkongwe nchini Amri Athuman 'King Majuto' aliyefariki dunia Agosti 8,2018 usiku unatarajiwa kuagwa leo Alhamis Agosti 9,2018 katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam kisha kusafirishwa kwenda Tanga kwa ajili ya Mazishi siku uya Ijumaa Agosti 10,2018.

UTARATIBU WA KUMUAGA MZEE WETU KING MAJUTO. 

Mwili wa Marehemu Mzee wetu Majuto utaswaliwa na kuagwa katika Msikiti uliopo pale ndani Muhimbili wakati wa Swalat Dhuhr (Swala ya Mchana). 

BAADA YA HAPO MWILI UTAAGWA VIWANJA VYA KARIMJEE DAR. 

HIVYO, Kuanzia saa nane Mchana Wanafamilia wote, ndugu, jamaa na marafiki, Wapenzi na Wadau mbali mbali tunatakiwa tukutane pale kwa ajili ya Kusoma Dua na Kumuaga Mzee wetu. 


Baada ya Swalat L'laasir (Swala ya Alasiri ) Mwili wa Marehemu Mzee wetu Majuto utasafirishwa kwenda Mkoani Tanga na Maziko ni Ijumaa baada ya Swalat Dhuhr ( Swala ya Mchana ) Tanga Mjini.

Pia kutakuwa na Usafiri maalum kwa ajili ya Wasanii. 

Wote mnaotarajia kusafiri Mnaelekezwa kujiorodhesha kwa Afisa Habari wa TDFAA Kinondoni Bw. Masoud Kaftany. 

Michango yote itakusanywa na Kamati ya Matukio na Uratibu. 


By. Chiki Mchoma. 

Mwenyekiti/Uratibu.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.