Wednesday, August 8, 2018

Breaking News : MZEE MAJUTO AFARIKI DUNIA USIKU HUU

  Malunde       Wednesday, August 8, 2018

Muigizaji na Mchekeshaji Maarufu Nchini Tanzania Amri Athuman Maarufu King Majuto ' Mzee Majuto amefariki dunia usiku huu majira ya saa mbili wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.


Msanii huyo mkongwe Amri Athuman maarufu kama " King Majuto" amefariki dunia usiku huu majira ya saa mbili leo Jumatano Agosti 8,2018  katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa mara tu baada ya kurejea nchini kutoka nchini India alikopelekwa na serikali kwa matibabu.

Msanii maarufu mhekeshaji Joti ndiye alikuwa mtu wa kwanza kutoa taarifa hizo za kusikitisha katika mtandao wake wa Instagram, ikiambatana na picha yake akiwa na msanii Mpoki walipokwenda kumjulia hali hospitali.

Joti ameandika kwenye ukrasa wake wa Instagram: “R.I.P @Kingmajuto. metuachia Maumivu Makubwa sana ktk Tasnia ya Comedy Tanzania Sisi wanao,Tutakukumbuka kwa kazi zako,Upendo wako,Tabasamu lako Daima milele,Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi,Pumzika kwa Amani Mzee wetu,” ameandika Joti.

Mwigizaji nyota wa vichekesho Steve Nyerere naye kwa masikitiko makubwa amethibitisha habari hiyo kwa kusema: "Kweli kaka, Mzee wetu katutoka. Tunalia kwa kumpoteza Mzee wetu..."

Muigizaji huyo alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, huko huko Tanga. Alianza fani ya kuigiza akiwa na umri mdogo wa miaka tisa, na toka wakati huo amekuwa kileleni katika fani ya uigizaji hadi mauti yalipomkuta.

R.I.P KING MAJUTO!
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post