KAULI YA SERIKALI KUHUSU MWANAFUNZI ALIYEFARIKI KWA KIPIGO CHA MWALIMU | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, August 29, 2018

KAULI YA SERIKALI KUHUSU MWANAFUNZI ALIYEFARIKI KWA KIPIGO CHA MWALIMU

  msumbanews       Wednesday, August 29, 2018

Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako amezungumzia tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kibeta, mkoani Kagera Siperius Eradius akitaka vyombo vya usalama kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwalimu anayetuhumiwa.

Akizungumza leo Agosti 29 wakati wa Kongamano la Kimataifa la Hisabati linalofanyika Chuo Kikuu cha Aga Khan, Profesa Ndalichako amedai kusikitishwa na tukio hilo na kwamba Serikali haitamfumbia macho yeyote atakayebainika kuhatarisha usalama wa wanafunzi shuleni, wakiwamo walimu wao.

Amesema mwalimu aliyesababisha mauaji hayo hakutumwa na mtu isipokuwa utashi wake.

Profesa amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati vyombo vya usalama vinapofanya kazi yake na kwamba tukio hilo lisitoe tafsiri kuwa shule siyo mahali salama kwa watoto.

Shule ni sehemu ambayo ni salama kwa hiyo asitokee mtu akafanya vitendo ambavyo hata wazazi wajiulize harugusu mtoto kwenda shule au asiende lakini serikali itachukua hatua kwa mtu yeyote atakayefanya shule ionekane si mahali salama‘-Waziri Ndalichako

Siperius (13) anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na mwalimu akituhumiwa kuiba pochi ya mwalimu
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post