Wednesday, August 29, 2018

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAOMBWA KUONDOA KERO YA KUKOSEKANA KWA VIFARANGA WA KUKU BORA NCHINI

  msumbanews       Wednesday, August 29, 2018


.
Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi ABDALLAH ULEGA akimkabidhi Vifaranga bora mmoja wa wachama chama cha Wafugaji Kuku Bora Mkoani DODOMA -CHAWAKUBODO mapema leo mjini Dodoma,kuku hao wametolewa na kampuni ya AKM GLITTERS,huku Mlezi wa Chama hicho CHAWAKUBODO Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akishuhudia

Makabidhiano ya Vifaranga bora kwa Chama cha Wafugaji Kuku Bora Mkoani DODOMA -CHAWAKUBODO,yakifanyika kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho kutoka kwa viongozi wa mkoa wa Dodoma akiwemo mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh.Patrobas Katambi. 
Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi ABDALLAH ULEGA,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh.Patrobas Katambi pamoja na Mlezi wa chama cha Wafugaji Kuku Bora Mkoani DODOMA -CHAWAKUBODO wakionesha vifaranga bora kwa wanachama wa CHAWAKUBODO,vifaranga hivyo vimetolewa na kampuni ya AKM GLITTERS.

Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi (MB) Abdallah Ulega akizungumza mapema leo kwenye hafla fupi ya kukabidhi Vifaranga bora kwa wachama wa chama cha Wafugaji Kuku Bora Mkoani DODOMA -CHAWAKUBODO mapema leo mjini Dodoma,kuku hao wametolewa na kampuni ya AKM GLITTERS


Waziri Mkuu Mstaafu MIZENGO PINDA ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuondoa adha ya kukosekana kwa vifaranga wa kuku bora nchini, sambamba na uhaba wa upatikanaji wa chakula bora cha kuku.

PINDA ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Wafugaji Kuku Bora Mkoani DODOMA -CHAWAKUBODO amesema hayo leo Jijini DODOMA wakati chama hicho kikipokea msaada wa vifaranga vya kuku bora kutoka Kampuni AKM GLITTERS, ambapo amebainisha kuwa ukosefu wa vifaranga na chakula bora cha kuku imepelekea wafugaji kukosa ari ya kuendelea kufuga.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi ABDALLAH ULEGA amekiri kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa chakula bora cha kuku nchini na kusema kuwa suala hilo ni lazima lishughulikiwe ili kumaliza tatizo hilo kwa wafugaji wa kuku .Pia Naibu Waziri ULEGA amebainisha kuwa kukosekana kwa vifaranga bora nchini kumetokana na udhibiti wa uingizwaji holela wa vifaranga vya kuku na kubainisha kuwa hivi sasa tatizo hilo lipo katika hatua za utatuzi na kwamba hali ya upatikanaji wa vifaranga itarejea kama zamani.

"Tumekubaliana lazima kuwe na udhibiti wa utotoleshaji wa vifaranga kiholela na utengenezaji wa vyakula vya mifugo jambo litakalosaidia kuondoa tatizo la kuwa na vifaranga na vyakula visivyo na ubora" alisema Waziri Ulega.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjinj PATROBAS KATAMBI amewapongeza wafugaji hao na kusema kuwa kwa sasa sekta ya ufugaji inakua hivyo ni lazima changamoto zilizopo ziweze kutatauliwa. Chama cha Ushirika wa Wafugaji Kuku Mkoa wa DODOMA kimepokea msaada wa vifaranga elfu nne ikiwa ni awamu ya kwanza ya msaada huo
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post