Thursday, July 19, 2018

SIMBA: “YANGA WANATUIGIZIA”

  mtilah       Thursday, July 19, 2018
Wakati ikielezwa kuwa beki ambaye bado hajasaini mkataba mpya na klabu ya Yanga, Kelvin Yondani kutajwa kuelekea upande wa pili, uongozi wa Simba umekana kuhusika na mipango hiyo.
 
Akizungumza na www.eatv.tv  Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema hakuna ukweli wowote kuhusiana na taarifa hizo huku akidai kuwa ni muvi ambayo Yanga wanaitengeneza wenyewe.
 
Manara amesema Yanga wameamua kuvujisha taarifa hizo wenyewe akisema wanajichanga kusaka pesa ili baadaye wakishamsajili waje kusema wameipiga bao Simba.
 
"Ni muvi ambayo Yanga wanaitengeneza wenyewe, wameamua kuvujisha taarifa hizo makusudi wasake pesa kisha wakija kumsajili waseme wameipiga bao Simba. Sisi hatumuhitaji wala hatuna mpango naye”, amesema Manara.
 
Manara amesema kuwa hawamuhitaji Yondani wala hawana mpango naye tofauti na taarifa zilivyosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuwa Simba ipo kwenye harakati za kumalizana naye.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post