MANARA ADAI YANGA WAMEIFEDHEHESHA TANZANIA, AMUOMBA RAIS MAGUFULI AINGILIE KATI
Thursday, July 19, 2018
Msemaji wa klabu ya Simba,
Haji Manara amedai kuwa klabu ya Yanga imeifedhehesha Tanzania nchini
Kenya usiku wa kuamkia leo kwa kukubali kipigo cha goli 4-0. Manara
akikazia hoja yake amesema Yanga wanatumia fedha nyingi za kigeni hovyo
kwa miaka yote jambo ambalo halileti maana kwani klabu hiyo imekuwa
ikivurunda kwenye michuano ya kimataifa huku akimuomba Rais Magufuli
aingilie kati matumizi hayo mabovu ya fedha ndani ya klabu hiyo.
“Mhe.
Rais wangu wakati huu ukikimbizana na ujenzi wa Viwanda nchini na
kuinua Uchumi wetu..nakuomba pia utupie jicho na huku..kuna klabu kwa
miaka yote imekuwa ikitumia hovyo fedha za kigeni na kulitia aibu Taifa
letu leo Wameifedhehesha Nchi.“ameandika Manara kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Klabu
ya Yanga jana imekubali kipigo cha mbwa koko cha goli 4-0 dhidi ya Gor
Mahia ya Kenya kwenye mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Kombe la
Shirikisho barani Afrika.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin