KUTUMBULIWA KWA MWIGULU...POLEPOLE AMVAA ZITTO KABWE...NAPE AFUNGUKA

Baada ya Rais Magufuli kutangaza mabadiliko madogo katika Wizara kadhaa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuachwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe wameanza kuvutana mitandaoni kuhusu kuachwa kwa Mwigulu.


Kupitia mtandao wa wa Twitter Zitto Kabwe amemkaribisha, Dkt. Nchemba kwa kumwambia sasa ni wakati wake wa kuwatumikia wananchi na kwamba msimamo wake ndiyo uliomponza.

"Ndugu yangu Mwigulu Nchemba karibu 'back bench' ufanye kazi ya Wananchi. Tunajua msimamo wako kuhusu barua ya KKKT umekuponza. Ulikuwa msimamo madhubuti na ulisimamia haki" - Zitto

Kufuatia kauli hiyo, Humphrey Polepole katika ukurasa wake, ameamua kumvaa Kiongozi huyo wa ACT kwa kumuita mzee wa kurukia treni kwa mbele na kwamba Rais amefanya mabadiliko kutokana na dhamana aliyopewa na Katiba na si vinginevyo na kumtaka asipotoshe watu.

Polepole ameandika "Mzee wa kurukia treni kwa mbele ushaanza, mbona unapenda ubashiri na vitendo vya kilozi? Rais hutenda impendezavyo kwa dhamana aliyopewa Kikatiba".

Ujumbe wa Zitto Kabwe na Humphrey Polepole kwenye mtandao wa Twitter

"Sisi tuliohudumu kwenye Serikali na Chama tunajua na kuheshimu. Usijitaftize huruma kwa mtu. Acha kupotosha hiyo si siasa safi. SAD! " Polepole

Kwa upande wa Mbunge wa Mtama ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Nape Nnauye amemkaribisha kiongozi huyo na kumtaka waungane kuwatumikia wananchi.

"Cde Karibu Sana! Tuliolelewa humu ni kama Mwanzi, upepo ukivuma Mwanzi unalala, upepo ukiisha Mwanzi unasimama ukiwa imara zaidi! Tuwatumikie waliotupa kura!" Nape.
Ujumbe aliouweka Mbunge wa Mtama Nape Nnauye kwenye ukurasa wake wa Twitter

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527