Sunday, July 1, 2018

URUSI WAITWANGA UHISPANIA..KUCHEZA ROBO FAINALI KOMBEA LA DUNIA

  Malunde       Sunday, July 1, 2018

Kombe la Dunia Urusi 2018 litaendelea bila mabingwa wa makala mawili yaliyotangulia, 2010 na 2014.

Mabingwa wa 2010, Uhispania imeandamana na bingwa mwenza wa 2014 Ujerumani, waliowatangulia kwa kutoka hatua ya makundi.

Uhispania imelemewa baada ya kipa wa Urusi Igor Akinfeev kuzuia mikwaju miwili na kuipa Urusi ushindi wa 4-3.

Kiungo Jorge Merodio, maarufu Koke na mwenzake Iago Aspas walipoteza mikwaju yao licha ya kufika kitovu cha penalti kwa shamrashamra na madaha.

Wenyeji hao Urusi wametua Robo fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya pili tangu 1996 wakati walifika hatua ya Nusu fainali.

Warusi sasa wanamsubiri atakayefanikiwa kati ya Croatia na Denmark.

Mechi yao ya robo fainali itapepetwa uga wa Olimpiki wa Fisht, Sochi Jumamosi saba Julai.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post