MAPACHA MARIA NA CONSOLATA KUZIKWA KWENYE KABURI MOJA,MISALABA MIWILI

Pacha walioungana Maria na Consolata wanatarajiwa kuzikwa Jumatano katika makaburi ya viongozi wa dini ya Roman Katoliki, Tosamaganga Mkoani Iringa.

Pacha hao wanaandaliwa jeneza moja lenye mfumo wa watu wawili huku misalaba ikiwa miwili na kaburi moja.

Akizungumzia ratiba ya maziko ya pacha hao, leo Juni 4, Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Richard Kasesela alisema wapo katika hatua za mwisho za maandalizi ya mazishi hayo.

Amesema ibada ya kuaga mapacha hao itafanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha (Rucu) kuanzia saa mbili asubuhi kabla ya safari ya Tosamaga kwa ajili ya mazishi.

"Taratibu zinaendelea na tumekubaliana kutengeneza jeneza moja lenye mfumo wa watu wawili, tutakuwa na misalaba miwil lakini watazikwa kaburi moja," amesema.

Kasesela amesema kuwa tayari ndugu wa pacha hao kwa pande zote mbili wamewasili na kwamba saa kumi jioni watakutana tena kupanga bajeti ya msiba.

Chanzo: Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527