Balaa!! FISI WATAFUNA NG'OMBE WAWILI NDANI YA DAKIKA 45 MWANZA


Wakazi wa kitongoji cha Chang’ombe kijiji cha Iligamba, halmashauri ya wilaya ya Buchosa Mwanza wamejawa na taharuki baada ya fisi kuvamia katika makazi yao na kutafuna ngómbe wawili kijiji hapo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Juni 5,2018 saa nane usiku ambapo fisi hao walivamia nyumbani kwa Dominic Mgisa mkazi wa kitongoji cha Changómbe na kutafuna ngómbe hao.

Kwa mujibu wa Mgisa, fisi hao waliwatafuna ng’ombe hao na kuwamaliza ndani ya dakika 45.

“Niligundua kuwa mifugo yangu inaliwa na fisi baada ya kutoka nje kujisaidia, niliposogea nikaona fisi, nikaogopa wasije kunidhuru nikarudi ndani,” amesema

Baada ya kuona hivyo Migisa alisema alipiga kelele kuomba msaada kwa majirani lakini hakuna aliyejitokeza kumsaidia kwa kuwa wengi waliwaogopa wanyama hao.
Na Daniel makaka,mwananchi
Theme images by rion819. Powered by Blogger.