AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KWENYE MAKALIO GEITA


Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Panda Kinasa (36) anayetuhumiwa kuwa kinara wa utekaji watu ameuawa kwa kupigwa na risasi makalioni wakati akiwa chini ya ulinzi akijaribu kuwatoroka polisi baada ya kuwapeleka kwenye mashimo alikokuwa ametupa miili ya watu wawili wilayani Bukombe mkoani Geita.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amesema tukio la kwanza la utekaji lilitokea Machi 24,2018 ambapo kijana Leornad Samwel(18) alitekwa majira ya saa saba usiku.

Amesema tukio la pili ni kuhusu mwanamke Nkwimba Mwandu ambaye alitekwa siku hiyo hiyo majira kama hayo na kwamba watekaji walitoa namba za simu wakitaka watumiwe fedha za kumkomboa vinginevyo wanawaua watu hao.

Kamanda Mponjoli amesema,baada ya kuonesha mahali alipotupa miili ya marehemu mtuhumiwa huyo alimpiga kikumbo askari kwa lengo la kutoroka na walipojaribu kumpiga risasi ili kumuogopesha hakuwa tayari kusimama ndipo askari wakampiga risasi kwenye makalio na akafariki akiwa hospitalini.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.