AS ROMA KUJIZUIA KUHUSU NIGERIA


Bajaji iliyopambwa na rangi ya jezi ya Nigeria iliyotumiwa katika michuano ya kombe la Dunia

****
Klabu ya AS ROMA inayoshiriki ligi kuu ya nchini Italia imeonesha heshima yao na pongezi kwa timu ya taifa ya Nigeria baada ya kumalizika kwa mchezo wa mzunguko wa tatu, hatua ya makundi ya kombe la Dunia nchini Urusi .

Klabu hiyo imeandika ujumbe huo wa pongezi kupitia mtandao wa Twitter ambao ulisomeka;

“ Ni masikitiko kuwa safari imeisha kwa 'Super Eagle's na mashabiki wao machachari, mlikuwa na jezi nzuri zaidi ambazo zilipambwa na hali ya upambanaji na kujivunia kwenu . Tumetengeneza marafiki wapya ambao wengine watabaki na wengine wataondoka, lakini tunatumani siku moja tutaonana Roma au tutatembelea Lagos. #StillForzaSuperEagles “. Ulieleza ujumbe huo.

Nigeria imeondolewa katika michuano ya kombe la Dunia baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa Argentina ambayo ilikuwa inahitaji alama tatu ili iweze kufuzu hatua ya 16 bora. Goli lililouwa matumaini ya Nigeria kufuzu hatua inayofuata lilifungwa na mlinzi Marcos Rojo baada ya kuunganisha 'frikiki' ya haraka muda mfupi kabla ya kumalizika kwa mchezo huo.

Gumzo kubwa la mchezo huo ni Penalti ya pili ya Nigeria iliyokataliwa na teknolojia ya usaidizi wa video kwa mwamuzi (VAR) ambayo wengi wa wadau wanaijadili kuwa ilikuwa ni sahihi na wengine wanasema haikuwa sahihi na ilikuwa sawa kukataliwa.

Sasa Argentina itakutana na Ufaransa katika hatua ya 16 bora na katika mchezo huo pia gwiji wa zamani wa Argentina, Diego Maradona alikimbizwa Hospitali baada ya kuzidiwa kwa furaha ya ushindi muda mfupi baada ya timu yake kufunga bao la pili na mchezo kumalizika.

Matumaini ya Waafrika yamebakia kwa Simba wa Teranga (Senegal) ambayo ina alama 4 mpaka sasa na mchezo wa mwisho wa hatua hii ya makundi itacheza Alhamisi dhidi ya Colombia ambapo Senegal inahitaji ushindi au sare ili iweze kufuzu hatua ya 16 bora.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527