Tuesday, May 1, 2018

VIONGOZI KIGOMA KUHAMASISHA WANANCHI KUPELEKA WATOTO WAPATE CHANJO CHA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

  Malunde       Tuesday, May 1, 2018

Serikali  mkoani Kigoma imewataka viongozi mbalimbali kuwa mfano katika zoezi la kuhamasisha wananchi kupeleka watoto wao wenye umri chini ya miaka 14 kwenye chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.

Rai hiyo imetolewa  jana na Brigedia jenerali Marko Gaguti ambaye ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu , Emmanuel Maganga, wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo kimkoa iliyofanyika wilayani Buhigwe.

Alisema njia ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na kupata chanjo, kutokufanya ngono katika umri mdogo, kubeba ujauzito katika umri mdogo pamoja na kuwa na wanaume zaidi moja.

"Njia ya pili ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini dalili za awali ili kupata matibabu mapema,"alisema.

Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mwanamvua Mlindoko alisema katika wilaya yake kuna jumla ya watoto 1325 wenye umri kati ya miaka 9 hadi 14.

Alisema katika wilaya yake inatarajia kutoa chanjo kwa watoto 4974 na kwamba hadi kufikia Desemba mwaka huu watakuwa wametoa chanjo kwa watoto hao kwa asilimia 100.

Diwani wa kata ya Kazurambimba Nuru Kashakali, alisema amejitolea kuzunguka katika shule zote za msingi zilizopo katika kata yake ili kuwahamasisha watoto hao kujitokeza katika zoezi la kupatiwa chanjo.
Na Rhoda Ezekiel- Malunde1 blog


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post