MAONYESHO YA BUNGE PROPERTY EXPO YAWA KIVUTIO DODOMA


Kampuni ya Terranova imeandaa maonyesho ya milki kuu , nyumba na nyenzo za ujenzi katika viwanja vya bunge jijini Dodoma. 

Maonyesho hayo yamezinduliwa rasmi jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  mheshimiwa William Lukuvi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Waziri Lukuvi  aliupongeza uongozi wa Kampuni ya kizalendo inayoongozwa na vijana waliopata elimu katika vyuo vikuu vya hapa nchini kufikisha elimu kuhusiana na sekta nzima ya ardhi na kuiletea Tanzania mendeleo kutokana na rasilimali.

Aidha alitoa rai kwa wadau kulipa kodi halali katika uendeshaji wa shughuli zao ili kwenda sawa na kasi ya ukuaji kiuchumi kupitia mapato ya ndani.

"Sisi tumeanza na tutazidi kuhamasisha wawekezaji wafike Dodoma , ili adhma kuu ya serikali ya kuhamia Makao makuu ya nchi izidi kupata tija kwa maendeleo yetu" ,alisema mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Terranova Emil Sylvester.

Wadau mbalimbali wamejitokeza kuonyesha bidhaa mbalimbali katika sekta hiyo wakiwemo, Nabaki Afrika,Fumba developments, Ngorongoro conservativation,Alrais developers na taasisi ya mwanamke ardhi.

Theme images by rion819. Powered by Blogger.