RAIS MAGUFULI : ' NITAONGEZA MISHAHARA KWELI KWELI'

Katika hotuba yake leo kwenye maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa Mkoani Iringa, Rais Magufuli ameahidi kupandisha mishahara kwa kiasi kikubwa kabla hajamaliza awamu yake ya uongozi.

''Kipindi changu cha Urais hakitaisha kabla sijapandisha mishahara wafanyakazi. Na mimi nataka niwaeleze kupandisha kwangu kutakuwa si kwa elfu kumi, kutakuwa kupandisha kwelikweli'', amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameweka wazi kuwa alitamani sana mwaka huu kupandisha mishahara lakini baada ya kuona changamoto zilizopo ikiwemo kulipa madeni ya nyuma akaona azimalize kwanza kabla ya kupandisha.

Pamoja na hayo Rais Magufuli ameviomba vyama vya wafanyakazi na masharikisho yao, kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwasababu inaongozwa na walimu akiwemo yeye mwenyewe na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambao wote wamewahi kuwa walimu.

Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya, kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizo ambazo zimefanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527