Tuesday, May 1, 2018

SHIRIKA LA AGPAHI LAFANYA MKUTANO NA WADAU WA UKIMWI MKOANI MWANZA

  Malunde       Tuesday, May 1, 2018
Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI), limewakutanisha wadau wa mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi mkoani Mwanza ili kwa pamoja kujadili na kuboresha shughuli mbalimbali zinazofanywa na wadau hao.

Afisa Mradi Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI mkoani Mwanza, Cecilia Yona amesema huo ni mkutano wa robo mwaka na unawashirikisha wadau wanaotoka katika vikundi vya kijamii (CBO) vinavyosaidia mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.

Amesema lengo la mkutano huo ni kusikiliza na kujadili shughuli mbalimbali zinazofanywa na wadau hao na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za tiba na matunzo kwa wateja wanaopata huduma katika vituo vya CTC.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wamebainisha kwamba wamekuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha wanawahamasisha wanajamii kuwa tayari kupima virusi vya Ukimwi na pia kuondokana na hali ya unyanyapaa.

Mkutano huo wa siku mbili kuanzia jana April 30, 2018 unafanyika Adden Palace Hotel Pasiansi Jijini Mwanza, ukihusisha washiriki kutoka wilaya za Nyamagana, Ilemela, Ukerewe pamoja na Sengerema ambapo shirika la AGPAHI limekuwa likifanya shughuli zake hapa nchini kwa ufadhili wa serikali ya Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control (CDC).

George Binagi-GB Pazzo @BMG
Afisa Mradi Huduma Unganishi kwa Jamii kutoka shirika la AGPAHI mkoani Mwanza, Cecilia Yona akizungumza kwenye mkutano huo. Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi wilaya ya Nyamagana, Erica Steven akizungumza kwenye mkutano huo. Washiriki wa mkutano huo. Bonyeza HAPA kwa habari zaidi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post