MVUA KUBWA KUNYESHA KWENYE MIKOA 17...TMA YATAHADHARISHA


Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa juu ya wastani, kwa siku tano zinazoweza kusababisha mafuriko katika maeneo mengi nchini.


Kwa mujibu wa TMA, mvua hizo zitaanza leo Mei Mosi mpaka Mei 5 mwaka huu na zinatarajiwa kunyesha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mikoa mingine ni Mara, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Katavi, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

TMA imesema kiwango cha athari zinazoweza kutokea katika jamii ni pamoja na adha ya usafiri, barabara kubwa kutopitika na maji kujaa au kupita kwa kasi.

Pia imetoa wito kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa.

Na Pamela chilongola,Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527