Tuesday, May 1, 2018

MUME AJIUA BAADA YA KUKIMBIWA NA MKEWE GEITA...HUU HAPA UJUMBE WAKE

  Malunde       Tuesday, May 1, 2018
Mwanaume mmoja mkazi wa Katoro mkoani Geita aliyetambulika kwa jina la Maganiko Nunda amejiua kwa kunywa sumu kufuatia mgogoro ulioibuka baina yake na mke wake siku hivi karibuni huku chanzo cha mgogoro huo kikidaiwa kuwa ni unywaji wa pombe kupindukia uliosababisha mkewe kumkimbia.

Akisimulia tukio hilo, mtoto wa marehemu amesema baada ya kwenda kumsalimia baba yake (marehemu) alimkuta ameshafariki huku akitokwa na povu mdomoni na puani.

Marehemu aliacha ujumbe wa barua wenye maneno yasemayo kuwa “…Kwa kuwa nimekuwa kero kwa familia yangu nimeamua kujiua…”

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho japo hakueleza ni aina gani ya sumu ambayo marehemu alitumia kujiua. Jeshi hilo linaendelea na upelelezi wa tukio hilo kabla ya kutoa taarifa kamili kwa umma.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post