AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMNYONGA AKIDAIWA KUSALITI PENZI


Victoria Swai enzi za uhai wake
***
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia kijana aliyefahamika kwa jina la Nicholas Light (25) mkazi wa Mtaa wa Mahama Ilemela kwa kumnyonga mpenzi wake Victoria Swai (26).


Inadaiwa kijana huyo alifanya mauaji hayo kwa kumkaba shingo mpenzi wake huyo hali iliyopelekea kukosa hewa na baadae kufariki dunia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kudai tukio hilo limetokea katika jengo la Ekacliff ofisi ya Kilimanjaro Avitaion.

Katika tukio hilo polisi walifanya uchunguzi katika nyumba alipokuwa akiishi marehemu na mpenzi wake na kumkuta mtuhumiwa akiwa amejificha juu ya dari ya nyumba.

Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa alikuwa akimsaliti kimapenzi ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 30.04.2018


¨       MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MPENZI WAKE KWA KUMNYONGA HADI KUFA WILAYANI NYAMAGANA.
  

KWAMBA TAREHE 29.04.2018 MAJIRA YA SAA 17:40HRS JIONI KATIKA JENGO LA EKACLIFF OFISI YA KILIMANJARO AVIATION MTAA WA ISALAMILO KATA YA ISAMILO WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NICHOLAS LIGHT MIAKA 25, MCHAGA, MKAZI WA MTAA WA MAHAKAMA –ILEMELA NA MFANYABIASHARA WA SAMAKI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MPENZI WAKE AITWAYE VICTORIA SWAI, MIAKA 26, MCHAGA, MKAZI WA MTAA WA MAHAKAMA – ILEMELA, YALIYOTOKANA NA KUMNYONGA KWA KUMKABA SHINGO HALI ILIYOPELEKEA KUKOSA HEWA NA BAADAE KUFARIKI DUNIA  KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

AWALI INASEMEKANA KUWA MARAEHEMU ALIKUWA AKIFANYA KAZI KATIKA KAMPUNI YA KILIMANJARO AVIATION INAYOHUSIKA NA MASUALA YA ANGA, LAKINI PIA ALIKUWA AKIISHI PAMOJA NA MPENZI WAKE NYUMBANI KWAKE MTAA WA MAHAKAMA – ILEMELA. INADAIWA KUWA KATIKA KAMPUNI HIYO TAJWA HAPO JUU AMBAYO MAREHEMU ALIKUWA AKIIFANYIA KAZI, WAFANYAKAZI WALIKUWA WAKIINGIA KAZINI KWA ZAMU MMOJAMMOJA (SHIFT), NDIPO TAREHE TAJWA HAPO JUU MAREHEMU ILIKUWA ZAMU YAKE NA ALIINGIA KAZINI PEKE YAKE.

INASEMEKANA KUWA WAKATI MAREHEMU AKIWA KAZINI MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO AMBAYE NI MPENZI WAKE ALIFIKA OFISINI HAPO KISHA UKAZUKA UGOMVI KATI YAO ULIOPELEKEA MTUHUMIWA KUMNYONGA MAREHEMU KWA KUMKABA SHINGO NA BAADAE KUKOSA PUMZI HADI KUFARIKI DUNIA.  AIDHA BAADA YA MUDA KUPITA VIONGOZI WA OFISI HIYO WALIFIKA OFISINI HAPO  NA KUKUTAA TUKIO HILO NDIPO WALITOA TAARIFA POLISI AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO.

POLISI WALIFANYA UCHUNGUZI ENEO LA TUKIO NA K`UWEZA KUMNG’AMUA MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO, KISHA WALIKWENDA KATIKA NYUMBA ALIPOKUWA AKIISHI MAREHEMU NA MPENZI WAKE NA KUMKUTA MTUHUMIWA AKIWA AMEJIFICHA JUU YA DARI YA NYUMBA. MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO AMEKAMATWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.

CHANZO CHA MAUAJI HAYO INASEMEKANA KUWA NI WIVU WA KIMAPENZI, KWANI INADAIWA MTUHUMIWA ALIKUWA AKIMTUHUMU MAREHEMU KUWA ALIKUWA AKIMSALITI KIMAPENZI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATO POLE KWA NDUGU NA FAMILIA KWA MSIBA WALIOUPA MWENYEZI MUNGU AWATIE NGUVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU AMBACHO WANAPITIA. SAMBAMBA NA HILO PIA ANATOA WITO  KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI VIJANA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERA MKONI PINDI WANAPOKUWA KWENYE MIGOGORO AIDHA YA KIMAPENZI AU YA AIANA YOYOTE ILE KWANI NI KOSA KISHERIA, BALI WAFUATE TARATIBU ZILIZOPO KISHERIA ILI KUEPUSHA  VIFO NA MAJERUHI YA AINA KAMA HII AMBAVYO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527