MABINGWA WAPYA WA SOKA SIMBA SC WAZIDI KUNOGESHA USHINDI


Mabingwa wapya wa soka nchini Simba, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United kwenye mchezo uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida United.

Bao la Simba limefungwa na Shomari Kapombe dakika ya 23 kipindi cha kwanza na kuihakikishia Simba kucheza mechi 28 bila kupoteza hata mchezo mmoja msimu huu.

Pia timu hiyo ambayo ilikosa ubingwa tangu msimu wa 2012/13 imesherehesha ubingwa wake kwa ushindi baada ya kuupata siku ya alhamisi kufuatia Yanga kufungwa na Prison lakini leo wao wameupokea kwa kuifunga Singida United.

Simba sasa imefikisha alama 68 kileleni katika michezo 28 ikiwa imebakiza mechi mbili kuweza kumaliza msimu huu. Mshambuliaji nyota wa timu hiyo Emmanuel Okwi ameshindwa kuongeza bao leo kwenye uwanja wa Namfua.

Simba itaondoka kesho asubuhi mjini Siginda na kutua jijini Dodoma tayari kwa mchezo wa kirafiki kesho jioni dhidi ya Dodoma FC na ksiha jumatatu kutinga bungeni kwa mwaliko maalum.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.