BWAWA LABOMOKA NA KUUA WATU 44 KENYA

Hali ya kuhuzunisha imeikumba Kenya baada ya watu zaidi ya 44 kufariki baada ya bwawa moja mjini Nakuru nchini Kenya kuvunja kuta zake Jumatano usiku na kusomba mamia ya nyumba za wakazi waliokuwa karibu na eneo hilo.

Tukio hilo limetokana na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha na kusababisha zaidi ya lita milioni 20 za maji kufurika kutoka bwawa la Patel katika shamba la maua.

Juhudi za kuwatafuta manusura bado zinaendelea katika eneo hilo.


Theme images by rion819. Powered by Blogger.