LULU AANZA ADHABU KWA KUFANYA USAFI OFISI ZA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu Lulu ameanza kutumikia kifungo chake cha nje kwa kufanya usafi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani zilizopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma za jamii, Charles Nzase amesema Lulu anaungana na wafungwa wengine 10 wanaofanya usafi wa mazingira wizarani hapo.

Amesema kila siku mwigizaji huyo atatumia saa nne kusafisha mazingira kisha ataendelea na shughuli zake nyingine za ujenzi wa Taifa.

Ameongeza kuwa tayari msanii huyo alianza kutekeleza adhabu hiyo tangu jana na kwamba ataendelea mpaka atakapomaliza kifungo chake Novemba, mwaka huu.

“Atapumzika siku za Jumamosi na Jumapili au siku za sikukuu, hatakuwa peke yake kwa kuwa tayari hapa wapo wafungwa wengine tisa wanaofanya kazi za usafi wa mazingira,” amefafanua Nzase.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527