RAIS MAGUFULI 'AMKAZIA' KIJANA ALIYEOMBA NAULI..AMTAKA AKALIME | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, May 15, 2018

RAIS MAGUFULI 'AMKAZIA' KIJANA ALIYEOMBA NAULI..AMTAKA AKALIME

  Malunde       Tuesday, May 15, 2018
Rais John Magufuli amemnyima fedha kijana mmoja aliyemuomba kiongozi mkuu huyo wa nchi nauli, wakati alipokwenda kwa mamantilie eneo la Bandari Dar es Salaam kunywa chai muda mfupi, baada ya kumaliza ziara yake ya kushtukiza katika bandari hiyo.


Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mei 15, 2018 wakati akinunua mapapai na ndizi baada ya kukuta chai ikiwa imekwisha katika genge la mamantilie huyo, huku kijana aliyekuwa akimsaidia mama huyo kupiga hesabu za matunda hayo, kuchomekea suala la nauli.


“Nataka mapapai nikale na wenzangu pale. Wewe mama jumlisha bei ninunue tena wewe mhehe si ndio, unaona sasa mtani wangu wewe. Haya haya hapa shilingi ngapi?,” amesema Magufuli akiuliza bei ya mapapai na kujibiwa kuwa ni Sh22,000.


“Na hizi ndizi ni kiasi gani, sawa kwa hiyo hizi ndizi zote pamoja na mapapai ni Sh23,000 si ndio. Sasa mimi nakuongeza nakupa Sh30,000 kabisa, au hutaki hela yangu mama.”


Baada ya mama huyo kupokea kiasi hicho cha fedha, kijana huyo alimuomba Rais nauli, “mheshimwia rais naomba nauli.”


“Hakuna nauli hapa nenda kalime,” amesema Rais Magufuli na kuwafanya waliokuwepo eneo hilo kuangua kicheko.


Ni kama kijana huyo alirudia tena kuomba nauli kwani rais alisikika tena akisema, “hakuna cha nauli hapa.”
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post