ZARI THE BOSS LADY AMLILIA MASOGANGE...HII HAPA KAULI YAKE

WASANII na watu mbali mbali wenye ukaribu na tasni ya burudani wameendelea kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’, Zari The Boss Lady naye hajakaa kimya.


Zari ameeleza kuwa Masogange alikuwa akimtafuta kupitia simu kila mwezi akimuulizia maendeleo ya watoto wake ingawa hawakuwa marafiki sana. Kupitia mtandao wa Snapchat Zari ameandika;


"We were not friends as such but ever since you got my number you’ve been dropping me a text every month and i mean no month passed without you asking how are the kids. in peace sis." 


Kwa kiswahili;
“Hatukuwa marafiki sana lakini tangu upate namba yangu umekua ukinitumia meseji kila mwezi na hakuna mwezi uliopita haujauliza kuhusiana na watoto wanaendeleaje pumzika kwa amani dada”
Masogange enzi za uhai wake aliweza kutokea kwenye video za wasanii kama AY na Mwana FA, Belle 9, Tunda Man, Izzo Bizness na wengineo. 


Amefariki jana April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527