LIPULI YABAKI NA ALAMA 4 ZA SIMBA....YATOKA SARE YA 1- 1

Klabu ya soka ya Lipuli FC imekuwa timu pekee hadi sasa ambayo haijafungwa na Simba katika mechi zote mbili za ligi kuu ya soka Tanzania bara baada ya kutoa sare ya 1-1 katika mchezo wa mzunguko wa pili leo.

Katika mchezo huo ambao umemalizika jioni hii kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa, Simba walilazimika kuwa nyuma kwa bao moja lililofungwa na Adam Salamba dakika ya 31 hadi dakika ya 66 ambapo Laudit Mavugo alisawazisha bao hilo.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es salaam, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 huku bao la Lipuli likifungwa na Asante Kwasi kwa mkwaju wa adhabu ndogo. Kwasasa Kwasi ni mchezaji wa Simba.

Kwa matokeo hayo sasa Simba imeendelea kusalia kileleni ikiwa na alama 59, baada ya michezo 25, ikifuatiwa na Yanga yenye alama 47 baada ya michezo 22 huku kesho ikitarajiwa kuwa dimbani kucheza na Mbeya City.

Baada ya michezo ya wikiendi hii, mchezo unaofuta ni wa watani wa jadi ambao utapigwa April 29 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.