Saturday, April 21, 2018

MWILI WA AGNES MASOGANGE KUAGWA VIWANJA VYA LEADERS - DAR, KUZIKWA MBEYA

  Malunde       Saturday, April 21, 2018
Video queen maarufu Bongo Agnes Gerald maarufu Kama Masogange anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao jijini Mbeya ambako ndiko wazazi wake waliko.


Dada wa Agnes anayejulikana kama Emma Gerald, amesema mwili wa Agnes utaagwa jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders, na kisha kusafirishwa kuelekea mkoani Mbeya kwa mazishi

“Tutaaga kesho asubuhi saa 3 pale Leaders, na kisha tutasafirisha kuelekea Mbeya kwa mazishi”, amesema Emma Gerald.

Sambamba na hilo muigizaji Steve Nyerere ambaye yuko karibu na familia ya Agnes amewataka wasanii kujitokeza kwa wingi leaders jioni ya leo, ili kujadili utaratibu wa mazishi na mengineyo. 

Agnes Masogange amefariki jana April 20, kwenye hospitali ya Mama Ngoma baada ya kulazwa kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta kwa tatizo la pneumonia
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post