Sunday, April 22, 2018

MUME AUA MKE KWA RUNGU AKIMTUHUMU KUZAA WATOTO WA KIKE TU

  Malunde       Sunday, April 22, 2018

Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog Kigoma 

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Selina Simon (35) mkazi wa Kijiji cha Itumbiko Wilayani Kakonko,ameuawa kwa kupigwa rungu na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani na mume wake Ndimugwanko Mlovezi (30) mkazi wa Itumbiko aliyemtuhumu kwanini anazaa watoto wa kike tu.

Malunde1 blog imeambiwa kuwa mwanamke huyo amefariki dunia Aprili 20,2018 majira ya saa moja na nusu usiku na kuacha mtoto mchanga.

Akizungumza baada ya kufika nyumbani kwa marehemu huyo Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema kwa mujibu wa ndugu wa marehemu huyo wanadai alipigwa na mume wake akawa anaogopa kusema kilichomkuta  na baada ya siku mbili alizidiwa na kumwambia mama yake kuwa amepigwa.

Ameeleza kuwa baada ya kupelekwa hospitali, tarehe 20 Aprili mwaka huu alifariki dunia kutokana na maumivu aliyokuwa nayo baada ya kupigwa.

Kanali Ndagala amesema chanzo cha tukio hilo ni migogoro ya familia ambapo inasadikika mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuzaa watoto wa kike tu na kusababisha kuanza kumpiga.

 Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kigoma, Maltin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hulo na kwamba  mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la mauaji na atafikishwa mahakamani.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kutenda vitendo vya ukatili kwakuwa ni kisa kisheria.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post