TAARIFA MPYA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA - TMA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema hali ya mvua katika maeneo mengi ya nchi itapungua kuanzia usiku wa leo Aprili 21, 2018.

Taarifa ya TMA iliyotolewa jana imesema maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Pia, TMA imesema maeneo mengine ya mikoa yatakuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

“Matazamio kwa siku ya Jumatatu Aprili 23, 2018, mvua inatarajiwa kupungua katika maeneo mengi ya nchi,” imesema taarifa hiyo ya TMA
Theme images by rion819. Powered by Blogger.