Sunday, April 22, 2018

RAIS MAGUFULI AMLILIA AGNES MASOGANGE

  Malunde       Sunday, April 22, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia ya Agnes Gerald Waya kufuatia kifo cha mtoto wao Agness alimaarufu kama Masogange kilichotokea Ijumaa.

Rais Magufuli ametuma salamu hizo kupitia kwa Mwenyekiti Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri James na kusema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha binti huyo kwani kifo chake kinapunguza idadi ya vijana ambao ndiyo jeshi na watu ambao wanaweza kufikisha mbali taifa. 

"Kupitia jukwaa hili naomba nitoa salamu za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye leo amewasilisi mjini Dodoma lakini ameomba niwasilishe kwenu salamu za pole kwa kuondokewa na kijana mwenzetu, Mwenyekiti anafahamu nchii hii sisi vijana ndiyo warithi wa taifa hili sisi ndiyo tumebebe dira ya kulifikisha taifa ambapo tunadhani linafaa kufika hivyo anasikitishwa sana kuona katika jeshi kubwa kama hili la vijana tunapungukiwa na vijana wenzetu wanaondoka na kupunguza idadi ya askari wetu , naomba mpokee salamu za Mwenyekiti wetu" alisema Kheri James 

Mwili wa Agness Masogange utazikwa jijini Mbeya nyumbani kwa wazazi wake Mbalizi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post