ZIARA YA WAZIRI MPINA KWENYE MNADA WA PUGU


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Kuhaga Mpina akizungumza na wananchi katika Mnada wa Pugu, Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.

Na Bashir Nkoromo, Pugu
Serikali ameagiza shughuli mpya za ujenzi na nyingine za maendeleo ikiwemo kilimo katika Kijiji cha Bangulo Kata ya Pugu Stesheni kusimama kuanzia leo, kusubiri mgogoro wa eneo kati ya Kijiji hicho na Mnada wa mifugo wa Pugu upatiwe ufumbuzi.

Akizungumza na wananchi leo baada ya kutembelea maeneo ya mpaka wa Mnada huo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ametoa agizo hilo kunusuru hali ya fukuto la mapigano katika ya wafanyabiashara kwenye mnada huo kudai Wanakijiji hicho cha Bangulo kuvamia eneo la malisho.

"Baadhi yenu mmeonyesha hapa hati za kumiliki makazi, lakini pia tunafahamu kuwa eneo la Mnada lilikuwa na ukubwa wa ekari 190, hivi sasa limebaki eneo kama asilimia 20 tu ya malisho. Hali hii inaufanya Mnada huu kukosa sifa, hivyo wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa kudumu naagiza shughuli zote za ujenzi na kilimo zisimame kwanza kuanzia leo," alisema Mpina.

Waziri Mpina amewataka wananchi kuishi bila hofu akisema suala lao litapatiwa ufumbuzi ambao utakuwa wa kudumu.

Habari katika Picha
Sehemu ya eneo la Mnada wa Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, leo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimkaribisha kufanya ziara, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina alipowasili kwenye Mnada wa Pugu wilayani hummo, Dar es Salaam, leo
Waziri Mpina akimsalimia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alipowasili kwenye Mnada wa Pugu leo
Waziri Mpina akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kabla ya kuanza ziara
Sophia Mjema akimuongoza Waziri Mpina kwenye eneo la kufanya mazungumzo na uongozi wa Mnada huo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo
Mkuu wa Mnada wa Pugu Kevamba Samwel akizungumzia hali ya maendeleo na changamoto za Mnada huo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo akijibu baadhi ya changamoto zilizoelezwa na mkuu wa Mnada huo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akieleza anavyozijua na alivoanza kuzishughulia baadhi ya changamoto za Mnada huo hasa mgogoro wa arhi baina ya Mnada na Wananchi
"Naona mda unakwenda mbio, hebu tuanze utembeleaji mipaka..." akasema waziri Mpina huku akitazama saa yake
Waziri Mpina akijadiliana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kipi waanze kati ya kuzungumza kwanza na wananchi au kukagua mipaka
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo akiwa ameweka bakora begani wakati safari ya kukagua mipaka ikianza. Kushoto ni Katubu wa Mwenezi tawi la CCM Bangulo Kata ya Pugu Stesheni Loyce Hamisi
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (kushoto) akiongoza kupanda moja ya vilima vilivyo katika Kijiji cha Bangulo wakati akikagua mipaka ya kijiji hicho na Mnada wa Pugu leo

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema naye akijiandaa kupanda kilima hicho 
"Kwa hiyo hadi kulee ni eneo la malisho ya Mnada?" Waziri Mpina akiuliza maofisa aliofuatana nao. Wapili kushoto ni DC Mjema
Afisa wa Mnada akimpatia maelezo waziri Mpina kuhusu lilivyo eneo la malisho ya Mnada wa Pugu 
Kamanda wa Polisi wilaya ya Ilala Kamishna Msaidizi Salim Hamduni akiongoza msafara wakati wa kushuka baada ya Waziri Mpina kukagua badhi ya maeneo ya mipaka kati ya kijiji cha Bangulo na Mnada wa Pugu 
Kisha waziri Mpina naye akashuka kilima hicho
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri Mpina baada ya kutoka kukagua mipaka hiyo

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala edward Mpogolo (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri Mpina baada ya kutoka kukagua mipaka hiyo
Baadhi ya nyumba katika kijiji cha Bangilo kinachodaiwa kuvamia eneo la malisho ya Mnada wa Pugu. Kushoto ni Waziri Mpina 
"Wenyewe mpo?" Waziri Mpina akiuliza huku akichungulia kwenye geti la nyumba moja inayoonyesha kujengwa hivi karibuni ambayo inadaiwa kuwa miongoni mwa nyumba za wananchi wa kijiji cha Bangulo waliovamia eneo la malisho la Mnada wa Pugu.
Aloyce Malya mkazi wa Kijiji cha Bangulo akizungumza wakati waziri Mpina alipozungumza na wananchi kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya wanankijiji hicho na Mnada wa Pugu leo
Kisha Aloyce akatia hati yake ya umiliki wa ardhi na kumkabidhi waziri Mpina
Waziri Mpina akiipitia kwa makini hati hiyo baada ya kuipokea
Hati yenyewe kwa karibu
Waziri Mpina akizungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mgogoro wa mipaka kati ya wananchi na Mnada wa Pugu
Wananchi wakimsikiliza waziri Mpina 
Waziri Mpina akiwaaga baada ya mazungumzo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post