TRENI YA ABIRIA YAANGUKA UVINZA - KIGOMA ,21 WAJERUHIWA

Treni ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania iliyokuwa ikitokea mkoani Dodoma kwenda Kigoma imepata ajali katika eneo la Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza leo  jioni siku ya Jumatano Februari 28,2018.

Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na kusababisha mabehewa mawili kuanguka katika dimbwi dogo la maji. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Martin Othieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba chanzo ni injini na mabehewa mawili kuacha njia na kuanguka.

“Mabehewa mawili ya abiria na injini ndiyo vimeanguka, hakuna vifo majeruhi wapo 21 kati yao mmoja ndiye ameumia sana”, ameeleza Otieno.

Amesema jitihada za kuwapatia majeruhi hao huduma ya matibabu zinaendelea. 

Behewa kadhaa bado zimesalia kwenye njia yake baada ya kutokea kwa ajali hiyo. 

Na Editha Karlo- Malunde1 blog

Theme images by rion819. Powered by Blogger.