MWILI WA AKWILINA KUAGWA DAR ALHAMIS,KUZIKWA IJUMAA KILIMANJAROMaziko ya mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline yatafanyika Februari 23, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na MCL Digital, kaka wa marehemu, Moi Kiyeyeu amesema baada ya kikao cha familia, wamekubaliana kuwa Akwilina atazikwa mkoani humo baada ya kuagwa Februari 22, 2018 katika viwanja vya NIT, Mabibo jijini Dar es Salaam.

Akwilina aliyefariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema

“Tutamuaga ndugu yetu siku ya Alhamisi katika viwanja vya chuo cha NIT pale Mabibo na siku hiyo hiyo tutaanza safari kuelekea Rombo-Mashati Olele mkoani Kilimanjaro na mazishi tutafanya Ijumaa,” amesema Kiyeyeu.
Na  Herrieth Makweta, Mwananchi

Theme images by rion819. Powered by Blogger.