MWANAUME ALIYEBEBA DAWA ZA KULEVYA KWENYE MAKALIO BANDIA AKAMATWA

Polisi nchini Ureno wamemkamata mwanaume mmoja kwenye uwanja wa ndege huko Lisbon, ambaye alikuwa amebeba kilo moja ya cocaine kwenye makalio bandia.

Vyombo vya habari nchini humo vilisema kuwa raia huyo wa Brazil aliwasili kwa ndege kutoka mji wa Belém do Pará, kaskazini mwa Brazil.

Haijulikani ni vipi polisi walifanikiwa kugundia hilo.

Mwanamume mwingine ambaye anashukiwa kuwa angepokea dawa hizo alikamatwa kwenye kituo cha treni cha mji huo.

Wanaume hao watakabiliwa na kesi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya.

Mwezi uliopita polisi nchini Ureno na Uhispania walikamata cocaine ndani ya mananasi yaliyokuwa yamessfirishwa kutoka Amerika ya Kusini.
Chanzo- BBC
Theme images by rion819. Powered by Blogger.