JANGILI AUAWA KWA KULIWA NA SIMBA AKIWINDA WANYAMA

Moja ya habari kubwa wiki hii ni kuhusu mtu mmoja anayedhaniwa kuwa jangili katika hifadhi ya simba karibu na Mbuga ya Wanyama ya Kruger amevamiwa na kuliwa na kikundi cha simba akiwa katika shughuli zake hizo za uwindaji nchini Afrika Kusini.

Polisi katika eneo hilo wameeleza kuwa mtu huyo ameraruriwa vibaya na vipande vichache tu vya mwili wake ndiyo vimepatikana ikiwa ni pamoja na mabaki ya kichwa.

Wameeleza kuwa mpaka sasa haijajulikana mtu huyo ni nani lakini uchunguzi unaendelea. 

Hata hivyo wamegusia kuwa kumekuwa na ujangili kwenye hifadhi hiyo, ambapo mwaka jana simba walipewa sumu na kufa huku vichwa na kwato zao zikachukuliwa.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.