KAMPUNI YA TTCL YABADILISHWA RASMI KUWA SHIRIKA LA UMMA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, February 2, 2018

KAMPUNI YA TTCL YABADILISHWA RASMI KUWA SHIRIKA LA UMMA

  Malunde       Friday, February 2, 2018
Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Februari 1, 2018 imefanya mabadiliko na kuibadili kampuni ya simu ya TTCL kuwa shirika la Umma.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametangaza maamuzi hayo  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa mabadiliko hayo hayawezi kuathiri wateja wa TTCL


"Sasa tunatoka kwenye TTCL kampuni na kuwa shirika la Umma tunaamini saizi mtajipanga zaidi kwenye mambo ya usalama na uimarishaji mambo ya uchumi. Pia napenda kuwajulisha Watanzania kuwa mabadiliko haya hayatawaathiri kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zikitolewa na kampuni ya simu ya TTCL, huduma zote zilizokuwa zikitolewa kuanzia kwenye simu za mkononi, data, enternet, TTCL Pesa zote zitaendelea sasa kwa kiwango kikubwa zaidi" alisema Mbarawa


Mbali na hilo Mbarawa amewataka TTCL sasa kufanya jitihada za kwenda kukusanya madeni yake kwa wananchi mbalimbali ambao wanatumia huduma zao na kusema kuwa Serikali inatambua ina deni kwa TTCL na kuwa wao watalipa na wako tayari kulipa ila wanapaswa kuanza kwenda kudai fedha zao kwa wananchi mbalimbali na makampuni ambayo pia yanadaiwa na TTCL.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post