CHADEMA WALIMWA BARUA KUFANYA KAMPENI NYUMBA KWA NYUMBA KINONDONI

Wakati kampeni za uchaguzi jimbo la Kinondoni zikiendelea, Chadema wamepewa barua mbili za malalamiko na msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli kikidaiwa kuvunja kanuni za maadili ya uchaguzi.

Akizungumza  Februari 1, 2018 Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema wamepokea barua hiyo jana, yenye malalamiko yaliyotolewa na Chama cha Wananchi (CUF).

Katika barua hiyo, CUF inalalamika kuwa Januari 28, Chadema walifanya kampeni nyumba kwa nyumba katika eneo la Kigogo Mbuyuni hadi London Bar badala ya siku hiyo kuwa kata ya Ndugumbi kama ratiba inavyoonyesha.

Malalamiko mengine ni Chadema kudaiwa kutumia salama ya CUF katika majukwaa ya kampeni sambamba na kupamba bendera za chama hicho.

"Madai mengine ni kwamba viongozi wa CUF wanakuja katika mikutano yetu na kukaa meza kuu na kupanda katika majukwaa. Pia CUF wanadai Chadema inawatumia viongozi wao kupita nyumba kwa nyumba kuiombea kura Chadema wakiwa na sare za CUF,” amesema Kigaila.

Kwa mujibu wa barua hizo Chadema wanatakiwa kutoa maelezo ya utetezi kwa maandishi kuhusu tuhuma hizo ndani ya saa 48 baada ya kuzipokea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527