TUNDU LISSU : KWA VYOVYOTE VILE KITENDO CHA LOWASSA SIYO CHA KUNYAMAZIWA

Baada ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kumtembelea Rais Magufuli Ikulu Leo January 9, 2018 Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu ametoa mtazamo wake kuhusu suala hilo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Lissu amepost picha inayomuonesha Lowassa akiwa Ikulu na kuandika maelezo haya; “Na hatukatai kuzungumza na Magufuli kuhusu matatizo mengi na makubwa yanayoikabili nchi yetu.”

“Lakini ni muhimu na lazima viongozi wakuu wa chama washirikishane na washauriane kabla ya mazungumzo hayo. Na baada ya mazungumzo, ni lazima viongozi wakubaliane juu ya kauli za kutoa hadharani kwa umma ili wote tuwe kwenye ukurasa mmoja.

“Viongozi na wanachama wetu wanashambuliwa hadharani kwa mapanga na hata kwa risasi, kumsifia Rais ni kumuunga mkono yeye. Katika mazingira ya kesi nyingi za kutunga dhidi yetu, ‘kazi nzuri’ inayofanywa ina maana gani, kama sio kuhalalisha ukandamizaji tunaofanyiwa.


“Katika mazingira ambapo hata jumuiya ya kimataifa imeanza kuhoji mwenendo wa Rais Magufuli, kutoa kauli kwamba ‘anafanya kazi nzuri’ ni ‘kumtupia taulo’ la propaganda litakalomfichia madhambi mengi aliyowafanyia Watanzania katika miaka hii miwili.


“Kwa vyovyote vile, kitendo cha Lowassa sio cha kunyamaziwa au kuhalalishwa kwa hoja nyepesi nyepesi.”– Lissu




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527