Wednesday, January 10, 2018

NAPE NNAUYE : NAIKUBALI SERIKALI YA AWAMU YA TANO, NAAPA KUFIA CCM

  Malunde       Wednesday, January 10, 2018
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), amesema kuwa hana mpango wa kuhamia chama chochote cha upinzani na ataendelea kubaki ndani ya CCM.

Alisema hawezi kufanya uamuzi wa kuhamia katika vyama vya upinzani , huku akidai magari ya upinzani kwa sasa yanazidi kuzama na haijulikani yataibuka lini.

Kauli hiyo aliitoa mjini Songea wakati akimnadi mgombea Ubunge wa Songea kupitia CCM, DK. Damas Ndumbaro katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Bombambili mjini hapa.
 
Nape ambaye pia aliwahi kuwa katibu Mwnezi wa CCM, alisema kama kuna watu walidhani atakihama chama tawala CCM na kujiunga na upinzani wasahau.

Alisema matatizo ya chama humalizwa ndani ya chama na si kukihama kama walivyofanya wanachama wengine waliokimbia ndani ya CCM.

“Naikubali serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Jemedari DK. John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa. Ni serikali yenye viongozi imara na mimi naapa kufia CCM na sivinginevyo.
 
“Nasikia maneno maneno kutoka kwa baadhi ya watu wakisema Nape anataka kuhamia upinzani jambo ambalo siyo la kweli kuanzia leo watu hao waondokane na mawazo hayo,” alisema Nape
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post