BABU SEYA NA WANAE WAIBUKIA MAPINDUZI YA ZANZIBAR


Familia ya mwanamuziki Nguza Vicking 'Babu Seya' imeungana na Wazanzibari kwa ajili ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Maadhimisho hayo yaliyafanyika jana Ijumaa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwamo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Tayari Serikali imewatafutia studio ya kurekodi muziki familia familia hiyo baada ya kuonana na Rais John Magufuli Ikulu waliopokwenda kutoa shukurani. 

Mmoja mtoto wa Babu Seya, Michael Nguza maarufu kama Nabii Nguza aliliambia Mwananchi kuwa lengo la kwenda Zanzibar ni kusherekea maadhimisho ya mapinduzi hayo.

“Tumekuja kusherehekea sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar,” amesema Nabii Nguza.

Babu Seya na wanawe Johnson Nguza ‘ Papii Kocha na Nabii Nguza wameanza kuonekana hadharani mfululizo ikiwa ni baada ya kuonana na Rais Magufuli walikokwenda kutoa shukurani baada ya kuachiwa huru Desemba 9 mwaka jana.

Baada ya kuonana na Rais Magufuli siku zilizofuata wakiwa na , Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza walikwenda katika Studio za Wanene zilizopo Mwenge kwa ajili ya mchakato wa kuanza kufanya kazi zao.

Na Bakari Kiango, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527