Saturday, January 13, 2018

KIKAO CHA DHARURA CHA CHADEMA KIMEAHIRISHWA MPAKA KESHO JUMAPILI KWA SABABU YA MSIBA

  Malunde       Saturday, January 13, 2018Kamati Kuu ya Chadema iliyokuwa imepangwa kufanyika leo imeahirishwa hadi kesho.


Kikao hicho kimeahirishwa ili kutoa fursa ya viongozi na wanachama wa Chadema kushiriki mazishi ya Anna Mayunga ambaye ni mama wa mkurugenzi wa sheria wa chama hicho, , Peter Kibatala.


Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Januari 13, 2018, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amesema “ni kweli Kamati Kuu ilikuwa ikutane leo lakini imeahirishwa hadi kesho(Jumapili).”


“Tumeahirisha ili kutoa nafasi ya viongozi kushiriki mazishi ya mama yake Kibatala yanayofanyika leo(Jumamosi) Morogoro mjini na Kamati Kuu itakutana kesho(Jumapili) jijini Dar es Salaam.”


Mrema amesema marehemu Anna alifariki juzi Alhamisi baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba aliokuwa amejikinga na mvua zilizokuwa zikinyesha na kudai kwamba si pekee aliyefariki kuna wengine pia.


Amesema mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe tayari yupo mkoani Morogoro kuhudhuria mazishi hayo akiwa pamoja na viongozi wengine na wabunge.


Na Elizabeth Edward, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post