Picha : RAFIKI SDO YAKUTANISHA BARAZA LA WATOTO NA KAMATI YA UCHUMI,ELIMU NA AFYA MANISPAA YA SHINYANGA KATIKA KIKAO CHA USHAWISHI



Shirika la Rafiki Social Development Organization – SDO la mkoani Shinyanga limefanya kikao cha ushawishi cha Baraza la watoto wa manispaa ya Shinyanga na kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga.



Kikao hicho kimefanyika leo Alhamis Desemba 21,2017 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza katika kikao hicho,Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath alisema lengo ni kuwakutanisha watoto hao na wajumbe wa kamati hiyo ambao wanashiriki katika utengenezaji wa bajeti ya manispaa.

“Mradi wetu unatekelezwa katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini na Kahama Mji,lakini leo tuna watoto wa manispaa ya Shinyanga,kupitia kikao hiki watoto wanaeleza changamoto wanazokutana nazo zinazopaswa kuchukuliwa hatua ngazi ya manispaa ikiwa ni pamoja na kushawishi bajeti ya manispaa iwe na mlengo wa kusaidia watoto”,alieleza Kimath.

“Rafiki SDO na Shirika la Save the Children kwa kushirikiana na idara ya maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo nchini Sweden (SIDA) tuliamua kuunda baraza la watoto kutoka kata 17 za manispaa hii kwa lengo la kuongeza ushirikishwaji wa watoto katika kutoa maamuzi hususani masuala yanayohusu watoto”,aliongeza Kimath.

Alisema kikao hicho cha kamati ya uchumi,elimu na afya na baraza hilo la watoto linaloundwa na watoto waliopo shuleni na ambao hawapo shuleni itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza nguvu ya ushawishi katika utengenezaji wa bajeti inayomlenga mtoto.

Wakizungumza katika kikao hicho watoto walizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na uhaba wa madarasa,walimu na watoto wa kike kukosa vifaa vya kutumia wakiwa katika hedhi hivyo kuomba serikali na mashirika mbalimbali kuangalia namna ya kutoa pedi kwa wanafunzi shuleni.

“Wanafunzi wa kike wamekuwa wakikosa masomo wanapokuwa katika hedhi,wanakosa pedi hivyo kuona aibu kufika shuleni lakini pia tunahitaji kila shule iwe na vyumba maalum vya kujihifadhi watoto wa kike wanapokuwa katika hedhi”,alieleza Nancy Aloyce kutoka Shule ya msingi Mwenge.

Naye Sara Chacha kutoka shule ya msingi Ushirika alisema bado kuna changamoto ya uchafuzi wa vyoo vya shule unaofanywa na wananchi wanaopita katika maeneo ya shule kwani shule nyingi hazina uzio hali inayohatarisha afya zao.

 Mjumbe mwingine wa baraza hilo la watoto,Maeja Geofrey kutoka shule ya msingi Bugoyi A aliomba serikali kuwa na bajeti inayolenga kusaidia watoto kwani baadhi yao wanaishi katika mazingira magumu hali inayowafanya wakatishe masomo na kuwa watoto wa mitaani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Reuben Kitinya alisema kamati hiyo imezipokea changamoto za watoto na mapendekezo yao na watajitahidi kuhakikisha bajeti yao inalenga watoto.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KIKAO HICHO
Mwenyekiti wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Reuben Kitinya akifungua kikao cha ushawishi cha Baraza la watoto wa manispaa ya Shinyanga na kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna leo Disema 21,2017. Kushoto ni Katibu wa kamati hiyo Raymond Kilindo ambaye ni Afisa Mipango wa manispaa ya Shinyanga- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwenyekiti wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Reuben Kitinya akizungumza wakati kikao hicho ambapo alilipongeza shirika la Rafiki SDO kwa kuona umuhimu wa kuandaa kikao kwa ajili ya kuwapa nafasi watoto kueleza changamoto zinazowakabili mbele ya kamati hiyo.
Wajumbe wa Baraza la watoto manispaa ya Shinyanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Reuben Kitinya.
Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath  akielezea lengo la kikao cha ushawishi kati ya wajumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga na wajumbe wa baraza la watoto manispaa ya Shinyanga.
Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath alisema shirika hilo kwa kushirikiana na serikali ya manispaa ya Shinyanga limeona ni vyema kuwapa nafasi watoto kueleza changamoto zinazowakabili mbele ya kamati hiyo
Wajumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Shirika la Rafiki SDO Eliud Lazaro akitoa mwongozo wa majadiliano wakati wa kikao hicho
Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya watoto shule ya msingi UshirikaSara Chacha, akielezea kuhusu changamoto wanazokutana nazo.Kushoto ni Nancy Aloyce kutoka Shule ya msingi Mwenge
Maeja Geofrey kutoka shule ya msingi Bugoyi A akichangia hoja wakati kikao hicho ambapo alisisitiza umuhimu wa serikali kutenga bajeti inayosaidia watoto wakiwemo watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Mtoto Abdalah Said akichangia hoja wakati wa kikao hicho

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Mwanamsiu Dossy akizungumza katika kikao hicho
Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Shela Mshandete ambaye pia ni diwani wa viti maalum (CCM) akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Moris Mugini ambaye ni diwani wa kata ya Chamaguha akizungumza katika kikao hicho
Wajumbe wa baraza la watoto wakiwa ukumbini
Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga Hamis Ngunila ambaye ni diwani wa kata ya Kitangiri (Chadema) akichangia hoja katika kikao hicho
Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga Zena Gulam ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Shinyanga Mjini (Chadema) akizungumza katika kikao hicho
Mjumbe wa kamati ya uchumi,elimu na afya ya manispaa ya Shinyanga,Zuhura Waziri ambaye ni Diwani wa viti maalum tarafa ya Ibadakuli akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akizungumza katika kikao hicho
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527