Saturday, November 18, 2017

KIJANA AHUKUMIWA JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA BINTI WA MIAKA 15

  Malunde       Saturday, November 18, 2017

MAHAKAMA ya Wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu mkulima wa Kijiji cha Paramawe, Kulwa Dase (35) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15.

Akitoa hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, Ramadhan Rugemalila alisema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka pasipo kuacha shaka yoyote kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Alisema kufuatana na mwenendo wa kesi hiyo ambao mashahidi wanne walitoa ushahidi upande wa mashitaka, mshitakiwa alikutwa na hatia chini ya Kifungu cha Sheria Namba 130(1) & (2)(e) NA 131 Sura ya 16 ya Kanuni ya Adhabu.

Awali, Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi wa Polisi, Hamimu Gwelo uliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 12, mwaka huu.

Imeandikwa na Pety Siyame- Habarileo Nkasi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post