Saturday, November 18, 2017

MGOMBEA UDIWANI WA CHADEMA NA KAMPENI MENEJA WAKE WAPANDISHWA KIZIMBANI

  Malunde       Saturday, November 18, 2017

Mgombea udiwani kata ya Mhandu (Chadema), Godfrey Misana na kampeni meneja wake, Charles Chinjibela, wamepandishwa kizimbani kujibu shtaka la kujeruhi.


Misana (46) na Chinjibela (37) wanadaiwa kumjeruhi meneja wa kampeni za CCM katika kata hiyo, Thomas Warioba.


Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, mbele ya hakimu Ainawe Moshi wanadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 14,2017.


Akisoma mashtaka katika shauri hilo namba 540/2017, mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Elizaberth Barabara amedai leo Ijumaa Novemba 17,2017 kuwa washtakiwa walitumia visu na mawe kumjeruhi Warioba.

Kabla ya kuhamia CCM, Warioba alikuwa mwanachama wa Chadema.

Upande wa Jamhuri umeiomba Mahakama kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa kile ilichoeleza ni kwa usalama wao.

Ombi hilo la Jamhuri limepingwa na wakili wa utetezi, Gasper Mwanaliela.

Wakili Mwanaliela amesema dhamana ni haki ya wateja wake na kwamba, kuwanyima kutawazuia kushiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26,2017.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Moshi amesema Mahakama itatoa uamuzi kuhusu dhamana Novemba 21,2017.

Washtakiwa wamepelekwa mahabusu hadi siku hiyo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post