TAARIFA KUTOKA KENYA HALI YA MATIBABU YA TUNDU LISSU

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa amesema wamefika salama Nairobi nchini Kenya na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anaendelea vizuri na matibabu.

Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Mbunge Msigwa amewataka watu waendelee kumuombea Lissu aliyesafirishwa jana usiku kupelekwa kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan akitokea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Tlifika salma tuendelee kumuombe ndugu yetu Lisu , anaendelea vizuri na matibabu!

Katika hatua nyingine, Rais wa Chama cha Mawakili cha Kenya (LSK), Isaac Okero amesema wanachama wa Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki leo mchana wataenda kumjulia hali Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post