MWANAMKE ALIYEMHIMIZA MPENZI WAKE AJIUE AFUNGWA JELA MIAKA MIWILI

Michelle Carter na mpenziwe Conrad Roy

Mwanamke mmoja wa Massachusetts nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela kwa kumshawishi mpenzi wake wa kiume kujiua kupitia ujumbe wa simu ya mkononi na kumpigia simu.

Michelle Carter, ambaye sasa ana umri wa miaka 20, atatumikia kifungo cha miezi 15 baada ya muda wake gerezani na miaka mitano akifuatiliwa mienendo yake.

Carter alipatikana na hatia ya mauaji ya kutokusudia ya Conrad Roy, ambaye alijiua tarehe 13 Julai 2014.

Baba yake Roy aliiambia mahakama Alhamisi kwamba: " Familia yangu imevunjika moyo. Mwanangu alikuwa rafiki yangu mkubwa."

Bi Carter aliruhusiwa kuwa huru huku akisubiri kesi ya rufaa.

Alikabiliwa na hukumu ya miaka 20 , lakini mawakili wake walidai kuwa yeye na mpenzi wake walikuwa na ugonjwa wa akili.

Akiwa amevalia suruali nyekundu na shati la rangi ya maziwa, Carter alilia huku akiwa amekunja mikono yake huku akitazama chini wakati hukumu yake ilipotolewa.

"Vitendo vyake vilimuua Conrad Roy," mwendesha mashtaka aliiambia mahakama." Alimaliza maisha ya Roy kuyafanya yake kuwa mazuri ."

" Hajakubali kuwajibika," alisema. " Hajaonesha kujuta ."

Lakini wakili wa Carter alisema ilikuwa ni " hali ya kutisha ambayo anasikitishwa nayo sana ".

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post